Home SIASA Hatutatumia magazeti kutatua ugomvi na Rwanda- Uganda yafunguka
SIASA - July 8, 2019

Hatutatumia magazeti kutatua ugomvi na Rwanda- Uganda yafunguka

Waziri wa Kazi Ofisini ya Waziri Mkuu nchini Uganda,  Mary Karooro Okurut ameambia Balozi wa Rwanda nchini Uganda, Frank Mugambage kwamba ugomvi kati ya nchi mbili hautatolewa suluhisho kupitia magazeti.

Waziri Karooro amefunguka hayo wakati wa sherehe ya miaka 25 ya kujikomboa kwa Rwanda.

“ Uganda iliamua kutatua masuala ya ushirikiano bila kutumia njia za magazeti. Nataka kumjurisha yeyote kuwa tunafatanya juu chini kutoa suluhisho. Tunastahili kutia kikomo kwa yanayoharibu  ushirikiano wetu.” Waziri Karooro ameambia Mugambage

Kwa upande wa Rwanda, Barozi Mugambage amesema nchi yake itaendelea kuonyesha Uganda masuala yanayokabili raia wake nchini humo.

“  Tulionyesha masuala ambayo Uganda haijafanya lolote husika kama vile waasi wanaolenga kushambulia nchi. Hili n tatizo kubwa.”

Msuguano kati ya Rwanda na Uganda ulianza mwaka 2017 ambako Wanyarwanda walianza kukamatwa kwa shutuma za upelelezi.

Kwa sasa, kama ilivyotangazwa na viongozi nchini Rwanda, mamia ya Wanyarwanda wangali jelani nchini Uganda na wengine karibu elfu moja walifukuzwa nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Check Also

Wanyarwanda washauriwa kutokwenda nchini  DRC

Waziri wa Afya nchini Rwanda,  Dkt. Diane Gashumba amewashauri wananchi kutokwenda nchini …