Home HABARI MPYA Kusini: Ndugu wawili wafariki kwa kuanguka shimoni
HABARI MPYA - July 29, 2019

Kusini: Ndugu wawili wafariki kwa kuanguka shimoni

Watoto wawili ambao ni ndugu wameanguka shimoni la migodi ya dhahabu, wakafariki dunia Wilayani Nyamagabe, Kusini Rwanda.

Imeripotiwa kwamba mashima hayo yalichimbwa na watu kinyume na sheria katika migodi ya wakazi.

Malehemu ni Elia Mugabonake, 10, na Frank Ishimwe ambao walianguka shimoni lililojaa maji walipokuwa wakicheza.

Mjomba wao amesema waliochimba dhahabu huko walikwenda na kuacha wazi mashimo hayo.

Viongozi wa ngazi za chini wamehakikisha  ripoti hii na kusema waliochimba mashimo wametoroka na kumeanzisha oeperesheni za kuwakamata.

Imeripotiwa kwamba  pia walifariki watoto wengine wawili baada ya kuanguka shimoni.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Check Also

Wanyarwanda washauriwa kutokwenda nchini  DRC

Waziri wa Afya nchini Rwanda,  Dkt. Diane Gashumba amewashauri wananchi kutokwenda nchini …