Home HABARI MPYA Wanyarwanda washauriwa kutokwenda nchini  DRC
HABARI MPYA - August 2, 2019

Wanyarwanda washauriwa kutokwenda nchini  DRC

Waziri wa Afya nchini Rwanda,  Dkt. Diane Gashumba amewashauri wananchi kutokwenda nchini DRC juu ya Ebola.

Onyo hilo ni baada ya wagonjwa wanne kupatikan Mjini Goma, ambako ni karibu na Rwanda.

“ Ugonjwa wa Ebola  ni wa kuambukiza. Tunawashauri watu wasiende mahali kwenye ugonjwa huo.” Waziri Gashumba aliwambia jana watangazaji.

“ Mipaka haikufungwa, tunachowaeleza watu ni kwamba kuna ugonjwa huko.” Ameongeza

Pamoja na hayo, waziri amewataka wakazi wasivuke mpaka kinyume na sheria. Amewataka pia kutii mbinu zote za kujikinga Ebola kama vile usafi, n.k.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Check Also

Rwanda yafunga mipaka na DRC

Rwanda imeamua kufunga mipaka yake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) juu ya Ebola.…